TAARIFA

March 17, 2017
News
Leo kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kigoma ( RCC ) kinakutana chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Hili ni Kama Bunge la Mkoa na inakutanisha Wabunge wote wa mkoa, Mameya na Wenyeviti wote wa Mammlaka za Serikali za Mitaa, Wakuu wa Wilaya wote mkoani na Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.  Kwa mbunge yeyote makini hivi sio vikao vya kukosa kwani ndipo mnapata nafasi ya kuunganisha mawazo yote ya mkoa na kuyapigania bungeni.
March 17, 2017
Speech
Wananchi wa Kata ya Kagera, Leo pamoja na mambo mengine nitazungumza nanyi kuhusu Mradi mkubwa wa Umwagiliaji kwenye Delta ya Mto Luiche. Mradi huu upo kwenye kata yenu. Wakati wa kampeni niliwaahidi kwamba tutajitahidi kuendeleza Bonde la Mto Luiche ili kuzalisha chakula cha kutosha kwa kulisha mkoa wetu wa Kigoma, mikoa mengine nchini pamoja na nchi jirani.
March 17, 2017
News
Ukiwa mbunge wa zaidi ya kipindi kimoja unaweza kupima tofauti ya maendeleo ya wananchi kwa kiashiria cha matatizo ya wananchi unayoyapokea kwa kuyasikiliza.  Bunge la 10 wananchi wengi wa Kigoma waliokuja kuniona nyumbani au ofisini ( Mimi husikiliza wananchi wote wa majimbo yote ya Kigoma bila kubagua) walikuwa na malalamiko ya kiuzalishaji ( ama kutozwa kodi au ushuru mkubwa, kukosa pembejeo za kilimo za ruzuku ama kuomba fursa za kazi kwenye miradi mbali mbali ya umma au sekta binafsi).