Kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona
Jiunge na vuguvugu letu ili kuleta mabadiliko unayoyataka Tanzania: mabadiliko yanayotengeneza ajira, kuleta heshima na furaha kwa watu wake.
Tunachokisimamia
Dhima yetu ni kuleta mabadiliko yatakayoiendeleza Tanzania kwa kutengeneza maisha ya furaha na heshima kwa Watanzania wote. Mabadiliko haya yatafanikishwa kwa kuwa na:
- Uchumi unaokuwa na jumuishi ambao unatengeneza ajira.
- Huduma bora za kijamii na zinazopatikana kwa watu wote.
- Polisi yenye kuwalinda na kuwatumikia watu yenye kujali taaluma na ukweli.
- Muungano wa watu (siyo wa Serikali), ambao ni wa haki na uliojengeka katika misingi ya kuheshimu haki za binadamu.