Msimamo wetu juu ya afya ya viongozi wa umma upo dhahiri kwa kauli na vitendo. Ndio maana Mwenyekiti wetu alipougua, Chama na yeye mwenyewe binafsi tuliweka bayana kwa umma. Kiongozi wa umma ni mali ya umma.
Sisi ndio Chama pekee ambacho tuliweka wazi maradhi ya Mwenyekiti wetu wa Taifa alipopata Corona. Vyama vingine viige kutoka kwetu ili kuondoa sintofahamu kwenye jamii.
Najua watu wana hamu kumsikia Kiongozi wa Chama chetu Zitto Kabwe. Watamsikia wakati muafaka. Yeye huongea pale inapobidi tu.
Ado Shaibu.
Katibu Mkuu.
14 Machi, 2021.
Do you like this post?
Showing 1 reaction
Sign in with
Facebook Twitter