Ado Shaibu

Katibu Mkuu

Ado alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo kwenye Mkutano Mkuu wa chama uliofanyika Machi, 2020. Akiwa na miaka 35, Ado ni Katibu Mkuu kijana kabisa kwenye chama chochote cha siasa nchini Tanzania. Kama Katibu Mkuu, yeye ndiyo mtendaji mkuu katika chama na anawajibika na shughuli za kila siku za chama pamoja na kuandaa na kutekeleza kampeni za chama.


Uchaguzi wa Ado kama Katibu Mkuu wa chama ulituma ujumbe kwa vijana wote nchini Tanzania kwamba ACT-Wazalendo ni chama chao. Ulionesha kwamba ndani ya ACT-Wazalendo, umri si kikwazo cha kutochaguliwa kwenye nafasi yoyote ya uongozi wa chama hicho.


Ado amewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo ambapo aliweza kuubadilisha uwepo wa chama kwenye majukwaa mbali mbali, kuhakikisha kwamba sauti ya chama inasikika kwenye mambo yote ya msingi yanayotokeakwenye nchi. Ado pia amekuwa Mtazania wa kwanza kumshitaki Raisi wa nchi baada ya kumteua Mwanasheria Mkuu ambaye hakutimiza vigezo vilvyowekwa na Katiba ya nchi.


Ado amezaliwa Tunduru, ambao ni mji mdogo Kusini mwa Tanzania. Alijipatia elimu yake ya msingi na ya sekondari kutoka Shule ya Msingi ya Nanjoka na Shule ya Sekondari ya Frank Weston. Baadae alienda Ndanda High School wilayani Masasi kwa ajili ya elimu yake ya sekondari ya juu. Ado ana shahada ya Sheria aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Safari ya kisiasa ya Ado ilianzia Shule ya Sekondari ya Frank Weston ambapo alichaguliwa kama kiogozi wa taaluma shuleni hapo. Punde tu baada ya uchaguzi huo, alijiuzulu kwenye nafasi hiyo akikataa kufanya kazi chini ya wafanyakazi waliokuwa wakiwatesa wanafunzi kupitia adhabu ya viboko. Hapa ndipo shauku ya Ado ya kupigania haki ilipoanzia, na ni shauku hiyo iliyomshajihisha ajiunge na siasa.


Wakati akiwa chuo kikuu, Ado alichaguliwa kuwa Katibu wa Wanafunzi wa Sheria katika Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho. Katika jukumu hili, Ado alipambana kwa gharama kubwa kwa ajili ya haki za wanafunzi wa chuo walionyimwa mikopo na Bodi ya Elimu ya Juu Tanzania.


Harakati za Ado za kupigania haki zilimpelekea ajiunge na ACT-Wazalendo. Kama Katibu Mkuu, dhima yake ni kukikuza chama ili kiweze kupigania heshima na furaha kwa ajili ya watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK