Dorothy Jonas Semu

Makamu Mwenyekiti - Bara

Dorothy alichaguliwa kama Makamo Mwenyekiti - Bara kwenye mkutano wa chama uliofanyika Machi, 2020. Katika nafasi hii, ataongoza kambi ya ACT bara kwenye mipango na utekelezaji wa mikakati mingine ya chama

Dorothy amefanya kazi kama Katibu Mkuu wa chama, jukumu aliloliacha wakati wa mkutano huo wa chama wa Machi, 2020. Wakati wa uongozi wake kama Katibu Mkuu, ACT-Wazalendo kilikuwa moja kati ya vyama vya siasa vinavyokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika baada ya kupokea wanachama na wafuasi wapatao 400,000 baada ya Maalim Seif Sharif Hamad kujiunga na chama hicho.

Kabla ya kuwa Katibu Mkuu, Dorothy alifanya kazi kama Katibu wa Sera na Utafiti wa ACT-Wazalendo.

Akizaliwa na wazazi ambao ni watumishi wa umma mnapo mwaka 1975, Dorothy amekulia jijini Arusha na wilayani Kilimanjaro ambako baba yake alikuwa akifanya kazi. Huduma na kufanya kazi kwa bidii aliwekewa na wazazi wake akiwa bado mdogo sana.

Dorothy ana shahada ya uzamili kwenye Physiotherapy kutoka Chuo Kikuu cha Westerna Cape, Afrika Kusini. Amefanya kazi kama mtumishi wa umma kwa miaka 17, akitumikia nafasi kama vile Clinical Physiotherapist na Mratibu wa Udhibiti wa Ulemavu wa Ukoma katika Wizara ya Afya. Kwa sasa anafanya kazi kama mshauri kwenye kampuni binafsi, Fizio Limited, na kama mshauri anayejitolea kwenye Chama cha Ukoma Tanzania.

Mara ya kwanza Dorothy kukutana na hali ya kutokuwepo kwa usawa ilikuwa pale alipopata fursa ya kuhudhuria shule mbali mbali wakati akiwa mdogo, kwenye umri wa miaka sita na nane: shule za kimataifa na za kawaida. Dorothy anakumbuka kuona bwawa la kuogelea kwenye shule moja ya kimataifa na shule ya kawaida ikiwa na madarasa yaliyojaa vumbi. Ni hapo ambapo Dorothy aliamua kwamba lazima ashiriki katika juhudi za kuondokana na kukosekana huko kwa usawa, akisukumwa wakati huo na kutafuta sehemu nzuri ya kuchezea na vifaa kwa ajili ya rafiki zake katika shule ya kawaida.

Hamu ya kutaka kuboresha maisha ya watu haijawahi kumwondoka Dorothy. Kazi yake ya mwisho serikalini ilimpatia fursa ya kuzunguka kwenye kila kona ya nchi kutoa huduma kwa watu wanaoikosa - watu walioathiriwa na ukoma. Kwa kuitumikia jamii hii kwa miaka zaidi ya 10, Dorothy amesaidia kuboresha takwimu za kitaifa juu ya huduma za tiba zinazotolewa kwa kundi hili la wananchi.

Kujiunga kwenye siasa haikuwa kwa bahati mbaya, licha ya kuhitaji kulitoa muhanga jukumu lake kama mtumishi wa umma. Dorothy aliichagua ACT-Wazalendo baada ya kuisoma Katiba yake na kushuhudia dhamira ya chama kutatua matatizo ya ukosefu wa usawa na kufanya maisha kuwa bora kwa kila Mtanzania.

Uzoefu wake mkubwa umemuwezesha kukiongoza chama cha ACT-Wazalendo katika vipindi vigumu sana, ikiwemo kutishiwa kufutiwa usajili kama chama rasmi cha siasa. Kama Makamo Mwenyekiti, Dorothy anaendelea kubaki na ndoto yake ya kuona Tanzania inakuwa bora wakati wa uhai wake.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK