Tunachokisimamia

Huduma za Kijamii

Tutahakikisha tunatengeza mazingira ya upatikanaji sawa wa huduma za kijamii kwa wote. Mfumo wetu wa elimu lazima uendelezwe na kufanywa kuwa wa kisasa, tukitoa kipaumbele kwa sayansi na teknolojia ili kusaidia kuongeza nguvu ya ukuaji wa uchumi wetu.
Umahiri unahitajika ili kuhakikisha Tanzania inaweza kushindana na walio bora duniani, kuhakikisha kwamba tunazalisha wahitimu bora na wabunifu ambao si tu wanaweza kuajirika bali pia wanaweza kuuhudumia uchumi unaokuwa.
Uchumi unaokuwa unahitaji taifa lenye afya. Tutajitahidi kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za kiafya na kwa wote zitakazotolewa na vituo imara vya afya na vya kisasa. Kinga itakuwa ndiyo kipaumbele chetu lakini pia tutahakikisha kwamba tiba zitakazotolewa kwa wanaohitaji ni za ubora wa hali ya juu duniani.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK