Tunachokisimamia

Katiba Mpya, Muungano na Tawala za Mikoa

Ilani 2020: ACT Wazalendo- Katiba Mpya, Muungano na Tawala za Mikoa

Serikali itakayoongozwa na ACT Wazalendo na vyama washirika, ndani ya miaka miwili, itafufua na kukamilisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano kwa kuwashirikisha Watanzania kikamilifu. Katiba mpya itaainisha;

1. Muunganano wenye Usawa, haki, kuheshimiana na wenye mwafaka

Kumekuwa na changamoto katika kuendesha Muungano wetu baina ya Nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar. ACT Wazalendo inaona kunahitaji kuwa na mwisho wa manung’uniko, mivutano na athari zinazotokana na kutokuwa na mwafaka, wa namna Muungano wetu unapaswa kuwa na kudumishwa.

Serikali ya ACT Wazalendo itafanya mambo yafuatayo ili kuleta Muungano wenye Usawa na haki;

i) kufuatia Katiba mpya ya Muungano, kuhakikisha kuwa kunatungwa sheria zitakayoendana na mahitaji ya wakati chini ya msingi wa haki, heshima na usawa kama nchi mbili huru zilizoungana kwa hiari zao. Matokeo yake ni kuwa na muungano wa haki, uwazi na usawa kwa kufaidisha kila upande;

ii) Itahakikisha kwamba Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha yanatekelezwa ikiwemo kuanzishwa na kufanya kazi ipasavyo na haraka Akaunti ya Pamoja ya Fedha. Aidha, itadai malimbikizo yote ya haki za mapato ya Zanzibar kutokana na mapato ya ziada ya Muungano kama ilivyochambuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha; Itailipa Zanzibar malimbikizo ya mgawo wa Mapato ya Muungano kwa kutunga sheria maalumu ambapo kila Mwaka Serikali ya Muungano itailipa Zanzibar Shs Bilioni 660 ( Transfer to Zanzibar as a payment of its accumulated non payments of its share from Union revenues ).

iii) Itaanzisha mchakato ya kurejesha mamlaka kwa Zanzibar katika nyenzo muhimu za uchumi ikiwemo kodi, fedha, ushirikiano wa kimataifa Kwa mambo yasiyo ya Muungano, ili iweze kujenga uchumi imara unaoendana na mazingira na mahitaji ya uchumi wa visiwa na pia kuamua kuhusu mustakbali wao;

iv) Itairejeshea Zanzibar hadhi yake ya kuwa na dhamana na jukumu la kuamua juu ya masuala ya sera za kiuchumi ikiwemo pia kuratibu masuala ya mitaji ya uwekezaji. Hii itaifanya Zanzibar kuwa na mipango ya uhakika ya kiuchumi, kifedha na uwekezaji;

vi. Itahakikisha kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaipatia Zanzibar mgao wake wa kifedha wa asilimia 11.02 kama ilivyowekeza katika mtaji wa uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania.

2. Mihimili na Tawala za Mikoa

  • Itaainisha na kuimarisha misingi ya haki na usawa kisheria, na kuweka nyenzo madhubuti za kusimamia haki, usawa, na uhuru kwa raia wake.
  • Itaimarisha uhuru na uimara wa mihimili yote ya Serikali.
  • Itajali maslahi  mapana ya Taifa letu na kuimarisha uwajibikaji.
  • Itasimamia uwepo wa ‘Serikali ya Umoja wa Kitaifa’.
  • Itaimarisha mfumo b wa kuendesha Serikali za mitaa – kwa kuwezesha ugatuaji wa madaraka zaidi kwa Serikali za Mitaa kwa kufuta ngazi ya Wakuu wa Wilaya.
  • Itawapa wananchi haki ya kuchagua wakuu wa mikoa kuanzia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025

3. Uraia Pacha

  • Itatoa  haki ya kikatiba na kisheria kwa Watanzania kuwa na Uraia Pacha.
Rudi kwenye ilani

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK