Mto Mara: Tunataka Uchunguzi Huru!

SERIKALI IACHE MZAHA JUU YA UCHAFUZI WA MTO MARA NA ATHARI KWA WANANCHI NA MAZINGIRA

Tunataka Uchunguzi Huru!

Chama cha ACT Wazalendo kupitia msemaji wa kisekta ya Maji na Mazingira, tumepokea kwa masikitiko makubwa matokeo ya kamati ya kitaifa ya kuchunguza suala la uchafuzi wa mto Mara, iliyotolewa tarehe 19 Machi 2022. Tumekuwa tukifuatilia kwa karibu sana kuhusu matukio haya, tangu tulipopata taarifa ya kwanza kabisa mnamo tarehe 6 Machi 2022. Na baadaye kuona baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kusambaza vipande video vikionyesha athari za uchafuzi wa mto Mara na baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi.
Wananchi, Wadau wa Mazingira na yeyote anayefuatilia suala hili atabaini kuwa Serikali kupitia Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) inafanya mzaha na kuwakejeli wananchi walioathirika na uchafuzi wa Mto Mara. Sababu zinazopelekea chama chetu kuona Serikali inafanya mzaha na afya za wananchi wa Mara na Mazingira ni kama zifuatazo;

1. Ripoti ya kamati ya kitaifa ya uchunguzi wa uchafuzi wa mazingira ya Prof. Samuel Manyele iliyotolewa tarehe 19 Machi, ina taarifa zinazopishana sana na taarifa ya awali ya uchunguzi wa kimaabara. Hii inaleta mkanganyiko miongoni mwa wadau, wananchi na wataalamu kujua uhalisia na ukweli wa taarifa hizi mbili. Mnamo tarehe 12 Machi 2022 Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) ilijitokeza na kueleza kuwa uchunguzi wa awali wa kimaabara umebaini uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta na kukosekana kwa hewa ya Oksijeni kwenye maji ya mto Mara jambo lilisababisha samaki na viumbe maji kufa. Huku ripoti ya Prof Manyele ikionyesha sababu ni kuwepo kwa kinyesi cha ng’ombe zaidi ya tani 1.8 Milioni na mkojo lita bilioni 1.5.
2. KwamudawotewauchunguzihadisasahakunajitihadamadhubutizilizochukuliwanaSerikali kushughulikia wananchi walioathirika na uchafuzi wa mazingira wa mto Mara. Wapo walioathirika kwa kupoteza mifugo yao (kufa) kutokana na kunyweshwa maji mifugo yao katika mto huo, wapo wavuvi waliopoteza kipato kwa kuzuia shughuli za uvuvi kupisha uchunguzi. Wapo pia wananchi waliopata magonjwa ya milipuko kutokana na athari za uchafuzi.
3. Sababu zinazotolewa na kamati kuhusu madhara yaliyojitokeza ni ishara ya kupuuza athari kubwa wanazozipata wananchi katika vijiji vya Ryamisanga, Kirumi, Ketasakwa, Kwibuse na Marasibora. ACT Wazalendo imebaini kwamba Serikali inaficha kiini cha tatizo kwa kutoa taarifa za mkanganyiko kwa makusudi ili kupindisha ukweli.
Nini kinatakiwa kufanyika?
1. ACT Wazalendo tunaungana na wananchi wa Mara, Wadau wote wa Mazingira kuitaka Serikali iache mzaha kwenye kulishughulikia suala hili linalogusa maisha ya watu. Tunaungana na hoja za wadau wengine ndani na nje ya nchi wanaoona uchuguzi wa Serikali una acha maswali mengi na kuwatia zaidi wananchi wasiwasi.
2. Tunataka ufanyike uchunguzi upya kupitia taasisi huru ya uchunguzi. Matokeo ya uchuguzi yawekwe wazi mapema iwezekanavyo. Hatuwezi kuamini ripoti za uchunguzi wa Serikali kwa sababu zimeshaonyesha mkanganyiko wa taarifa zake.
3. Zichukuliwejitihadazamakusudinaharakazakudhibitiuchafuziuliojitokezakwakusafishamaji kutumia kemikali/dawa stahiki za kusafishia maji zinazotambulika na mamlaka ya usafishaji maji kwa matumizi halali ya binadamu, viumbe waishio majini pamoja na mimea na Wanyama
4. Serikaliitoefidiakwawananchiwotewaliopatamadharayanayotokananauchafuzihuowamaji na mazingira, kwa kuwapatia huduma za kiafya bure wananchi waliopata madhara ya kiafya na fidia kwa waliopoteza mifugo na ajira zao.
Mwisho, Chama cha ACT Wazalendo tunaelekeza masikitiko yetu makubwa kwa jinsi Serikali ilivyozembea kushughulikia tatizo hili liliothiri wananchi, mifugo yao na viumbe maji. Serikali haijaonyesha kujali maslahi ya wananchi wake na mazingira kwa ujumla. Tunaungana na wadau wote walioguswa na tatizo hili na hasa kwa wakazi wa Mara. Serikali inatakiwa kuweka wazi taarifa za tatizo hili ili lishughulikiwe kwa maslahi mapana ya taifa.

Imetolewa na:

Ester Thomas. Msemaji wa Sekta ya maji na mazingira. ACT Wazalendo. [email protected]
23 Machi, 2022
____________________________________________

Showing 1 reaction

Please check your e-mail for a link to activate your account.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK