PAZA SAUTI KUSAIDIA KUREJESHWA KWA WAGOMBEA WETU WALIOENGULIWA
Muda umewadia wa kusimama na kuidai haki yetu ya uchaguzi huru na wa haki.
Tutaendelea kudai kurejeshwa kwa wagombea wetu walioenguliwa na kwamba NEC na ZEC zichukue hatua za haraka kuhakikisha uchaguzi wa huru na haki.
Paza sauti hapa kudhihirisha kwamba unaunga mkono uchaguzi huru na wa haki.
Tukiwa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika 28/10/2020, watawala waliopo madarakani wanafanya kila wanaloweza kuzuia vyama vya upinzani kushiriki katika uchaguzi huo katika ngazi za majimbo na kata ambako wanajua chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM), kitashindwa vibaya.
Kwa kuwaengua wagombea wetu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) zinaisadia CCM kwa gharama ya vyma vingine washindani.
Jinsi hali ilivyo kwa sasa:
- Wagombea wa Ubunge katika ngazi za majimbo wameenguliwa katika mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Muungano katika pande zote mbili za muungano, Tanzania Bara na Zanzibar.
- Jumla ya wagombea uwakilishi 11 wamezuiliwa kushiriki uchaguzi wa kuwapata wajumbe wa Baraz la Wawakilishi Zanzibar.
- Wagombea udiwani pia wameenguliwa katika pande zote mbili za muungano, Tanzania Bara na Zanzibar.
Hakuna mgombea hata mmoja wa CCM “aliyeenguliwa.”
Badala yake, wagombea wa upinzani wameondolewa kwenye kinyang’anyiro kwa njia za kijinga, ikiwemo kutunga vikwazo, kubadilisha fomu za uteuzi zilibadilishwa na ukaataji wa mihuri halali ya mahakama na ile ya chama.
Bila ya uwakilishi toshelevu na mpana wa wanasheria wa upinzani, NEC na ZEC hazitakuwa tayari kuendesha uchaguzi wa huru na haki.
Muda umewadia wa kusimama na kuidai haki yetu ya uchaguzi huru na wa haki.
Tutaendelea kudai kurejeshwa kwa wagombea wetu walioenguliwa na kwamba NEC na ZEC zichukue hatua za haraka kuhakikisha uchaguzi wa huru na haki.
Paza sauti hapa kudhihirisha kwamba unaunga mkono uchaguzi huru na wa haki.
Kwa pamoja, tunaweza kujenga Tanzania yenye uchumi unaokuwa, wenye kutengeneza ajira, kuleta heshima na furaha kwa wote.