Tunachokisimamia
Polisi
Tanzania inastahili polisi yenye kujali taaluma na ukweli ili iweze kuwalinda na kuwahudumia watu wote.
Chini ya Serikali ya sasa, jeshi letu la polisi linatumika kama chombo cha Serikali, likiwa na lengo la kuwaadhibu maadui wa Dola. Jeshi la polisi kwa sasa linawatumikia wale tu waliopo madarakani.
Tutahakikisha tunajenga taasisi ya polisi ambayo ni huru na ambayo itakuwa tiifu kwa Katiba ya nchi na si kwa mtu au chama cha siasa.