TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KAIMU MWENYEKITI TAIFA WA ACT WAZALENDO

Kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Ndugu Maalim Seif Sharif Hamad kilichotokea tarehe 17 Februari 2021, Ndugu Dorothy Semu ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti Bara anakuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 84(3) na (4) ya Katiba ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015 Toleo la Mwaka 2020 inayosomeka kama ifuatavyo;

‘’84(3): Iwapo Mwenyekiti wa Chama hayupo kwa sababu yoyote ile basi Makamu Mwenyekiti ambaye anatoka upande mwengine wa Muungano tofauti na anaotoka Mwenyekiti, na kama Makamu Mwenyekiti aliyetajwa kwanza naye hayupo, basi Makamu Mwenyekiti aliyebakia atakaimu nafasi ya uenyekiti.’’

Aidha, kwa kuzingatia Ibara ya 84(4) ya Katiba ya ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu ataendelea kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) hadi pale Mwenyekiti Mpya atakapochaguliwa na Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa.

 

Imetolewa na:

Salim A. Bimani,
Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma,
ACT Wazalendo
22 Februari, 2021.

Showing 1 reaction

Please check your e-mail for a link to activate your account.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK