January 31, 2021 2:12 PM

TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

Chama cha ACT Wazalendo kinawajuilisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania, kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe, Bi Awena, pamoja na Wasaidizi wake kadhaa wa karibu, wamethibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi Madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalumu katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya Korona. Hivyo basi, tangu juzi Ijumaa jioni, Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa Madaktari.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa hali ya Maalim Seif pamoja na mkewe zinaendelea vyema kabisa, Viongozi wenzake pamoja na Wanafamilia wamekuwa na mawasiliano naye ya kawaida kila siku.

ACT Wazalendo tunawaomba wanachama wetu, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki ambacho amepumzishwa ili aweze kupona kwa haraka na arudi kuendelea na majukumu yake. Pia, tunarejea wito wetu kwa Watanzania wote kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.

 

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo
31 Januari, 2021.

Showing 1 reaction

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK