TUMESHAMPENDEKEZA MRITHI WA MAALIM -Zitto

(Sehemu ya Hotuba ya Kiongozi wa Chama Ndugu cha ACT Wazalendo Ndg. Zitto Kabwe kwenye Khitma ya Kumuombea Maalim Seif Iliyofanyika Dar es salaam).

"Tayari tumeshapendekeza jina kwa Rais wa Zanzibar la mtu ambaye atarithi majukumu ambayo Maalim Seif alikuwa anayafanya.

Bahati nzuri, Maalim alikuwa ni Kiongozi. Alijua kuna siku Mwenyezi Mungu atamchukua kwa sababu sisi sote lazima turejee kwa Mwenyezi Mungu kama tulivyoambiwa na mafunzo ya dini yetu na dini zote.

Kwa hiyo aliacha ametupa maelekezo ya nini kitokee iwapo atatangulia mbele ya haki.

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba viongozi wa Chama wamefuata yale maelekezo yake kwa namna ambayo Kiongozi wetu alituelekeza. Sasa umebaki wajibu wa Rais wa Zanzibar wa kuyatekeleza hayo.

Sisi tunaamini kabisa kuwa huyo ambaye amependekezwa ataweza kusimamia maridhiano na haki za Wazanzibari kama ambavyo Maalim Seif mwenyewe alikuwa akifanya.

Tunawaomba muendelee kutuombea dua ili tusitoke kwenye mstari, tuendelee kupigania demokrasia, haki na kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa ya amani ili iweze kupata maendeleo ya watu."

Showing 1 reaction

Please check your e-mail for a link to activate your account.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK