September 01, 2017 7:38 PM

UKAMATWAJI WA KIONGOZI WA CHAMA NDG. ZITTO KABWE NI UKIUKAJI MKUBWA WA SHERI

Mapema leo, Kiongozi wa Chama ndg. Zitto Kabwe pamoja na viongozi wengine 8 akiwemo Mbunge mstaafu wa Kilwa Kusini ndg. Seleman Bungara, Katibu wa Oganaizesheni na Wanachama wa ACT ndg. Shaweji Mketo na Mjumbe wa Kamati Kuu ndg. Isihaka Mchinjita wamekamatwa na polisi nje ya utaratibu wa kisheria.

Ndg. Zitto na ujumbe wake walikuwa katika kikao cha ndani katika ziara ya Kiongozi jimbo la Kilwa Kusini mkoa wa Lindi. Kikao hicho ni shughuli halali kabisa kisheria kama ilivyofafanuliwa na sheri ya vyama vya siasa.

Wakiwa wamedhamiria kuwatisha na kuwadhalilisha, polisi walivamia na kuvuruga kikao cha Kiongozi wa Chama na kushinikiza ukamataji wa viongozi hao waliokuwa wakiendelea na kikao katika hali ya amani na utulivu.

Baada ya kuwakamata wamewafikisha polisi na kuanza kuwahoji juu ya tuhuma za kuhamasisha na kufanya mkusanyiko batili.Hatua hiyo ni mwendelezo wa serikali ya CCM kuwatisha na kuvuruga ushindani wa kisiasa katika uchaguzi ujao ambao ni dhahiri wanauhofia.

Wiki mbili zilizopita Mwenyekiti wa Chama Taifa ndg. Seif Sharif Hamad alieleza juu ya masikitiko makubwa namna ambavyo vyombo vya dola vimejigeuza kuwa vyombo vyakulinda maslahi ya CCM jambo linalohatarisha uwepo wa uchaguzi huru na wa haki baadaye mwezi Oktoba mwaka huu.

Matukio haya ya leo ni mfano wa dhahiri namna ambavyo polisi inatumika na CCM kuzuia shughuli halali za vyama vya upinzani na kuwafungulia kesi zisizo na msingi viongozi na wanachama wetu.Polisi wanapaswa kujitambua kwamba wao ni watoa huduma, na siyo kikundi cha ubabe. Wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia haki za raia. 

Tunawataka polisi kufanya kazi zao kwa kufuata haki, utaratibu na bila kuegemea na kukandamiza upande wowote kwa kuzingatia sheria.Tunasimama imara pamoja na Kiongozi wetu wa Chama pamoja na viongozi wenzake wote waliokamatwa na tunafanya kila jitihada kuhakikisha wanaachiwa huru.

Aidha, tutaiandikia Tume ya Uchaguzi (NEC) kwani hili lililofanyika ni uvunjifu wa shughuli halali za vyama na tutaitaka ichukue hatua mara moja ikizingatiwa kuwa uchaguzi mkuu uko ukingoni.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK