Zitto Zuberi Kabwe

Kiongozi wa Chama

Zitto ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo na amehudumu kama Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini katika Bunge lililomaliza muda wake la 11.


Zitto ni mchumi kitaaluma, akiwa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Zitto pia alisomea Biashara ya Kimataifa kutoka Went-Trade Africa Programme (Bonn, Ujerumani) na ana Shahada ya Uzamili kwenye Sheria na Biashara aliyoipata kutoka Shule ya Sheria ya Bucerius (Humburg, Ujerumani).


Akiwa amefanya kazi kama Mwenyekiti wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Uwekezaji wa Serikali, Zitto amejipambanua kuwa mpigania uwajibikaji, uwazi na utawala wa sheria nchini Tanzania.
Zitto ameweza kuwashajihisha vijana wengi nchini Tanzania kujiunga na siasa, na amekuwa mstari wa mbele katika kuchochea mabadiliko kwenye sekta ya madini, akipigania uwazi wa mikataba katika mali asili na kuzuia utoroshwaji wa fedha nje ya nchi.


Mwezi Julai, 2015, jarida maarufu ulimwenguni la masuala ya biashara la Financial Times lilimtaja Zitto kwenye orodha yake ya watu 25 wa Kiafrika wa kuwaangalia.
Zitto ni mwanasiasa aliye na wafuasi wengi katika mtandao wa kijamii wa Twitter akiwa na watu zaidi ya milioni moja wanaomfuatilia.

 

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK