JESHI LA POLISI LIMUACHIE WAKILI PETER MADELEKA: HOJA ZAKE DHIDI YA UHAMIAJI ZIJIBIWE KWA HOJA NA SI VITISHO NA UKAMATAJI.

JESHI LA POLISI LIMUACHIE WAKILI PETER MADELEKA:
HOJA ZAKE DHIDI YA UHAMIAJI ZIJIBIWE KWA HOJA NA SI VITISHO NA UKAMATAJI.

Chama cha ACT Wazalendo kinalitaka Jeshi la Polisi kumtendea haki kwa mujibu wa Sheria Wakili Peter Madeleka kutokana na kumkamata kinyume na taratibu siku ya jana 20.04.2022 katika Hotel ya Serena jijini Dar es salaam na kumshikilia pasina kuruhusu ndugu wala wanasheria wake kuonana naye.

Tukio hilo limetokea jana katika Hoteli ya Serena kwa watu wanaosadikiwa ni maafisa wa Jeshi la Polisi wasio na Utambulisho wowote na gari lisilo na namba za usajili wa polisi kufika hotelini hapo na kumchukua wakili huyo bila kufuata taratibu za kisheria. Baadaye, baada ya ndugu na jamaa wa karibu kufuatilia, ndipo Polisi walikiri kumshikilia.

Siku za hivi karibuni, Wakili Peter Madeleka amekuwa akiishinikiza Serikali kuwachukuliwa hatua maafisa wa uhamiaji waliofanya ubadhilifu wa utengenezaji wa stika feki za viza kama ambavyo mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) alivyobainisha kwenye taarifa yake ya uakaguzi wa 2020/2021. Wakili Madeleka hivi karibuni alianza kupokea vitisho vya kuuwawa na watu wanaosadikika kuwa maafisa wa uhamiaji. Hatimaye amekamatwa bila kosa lake kubainishwa na Polisi.

1. ACT Wazalendo tunataka wakili Peter Madeleka aachiwe huru bila masharti sababu hakuna kosa zaidi ya hujuma dhidi yake. Hoja za CAG dhidi ya Uhamiaji zijibiwe kwa hoja.

2. ACT Wazalendo tunataka Wakili Peter Madeleka apelekwe Mahakama ndani ya muda mfupi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi ili kuthibitisha kama kuna mashitaka dhidi yake,

3. Wakili Peter Madeleka atendewe haki za kisheria kuonana na familia na Wanasheria wake, hatua zake za kutoa taarifa za kutishwa kuuwawa siyo kosa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Tunatoa wito kwa Jeshi letu la Polisi kuhakikisha linatekeleza majukumu yake kwa weledi na kufuata sheria, kuzingatia haki za binadamu na lisiturudishe katika miaka 6 iliyopita ya zama za GIZA.
Imetolewa na; Ndugu. Mbarala Maharagande, [email protected]
Msemaji wa ACT Wazalendo - Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Showing 1 reaction

Please check your e-mail for a link to activate your account.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK