Tunachokisimamia

Uchumi

Jamhuri yetu ya Muungano lazima iwe na uchumi wa kisasa, wenye mafanikio na uliopanuka na unaoweza kutengeneza ajira. Kama taifa, tuna fursa ya kustawi na kumtoa kila mmoja wetu kutoka kwenye dimbwi la umasikini. Lakini Serikali ya sasa inasimamia uchumi dumavu na unaosuasua katika ukuaji wake na hivyo kuendelea kuwafukarisha watu.
Tutajenga uchumi imara, unaokuwa na jumuishi utakaosimama juu ya misingi ya uwekezaji kutoka nje, ukuaji wa sekta mahususi na kuifanya Tanzania kuwa mlango wa kuingilia Afrika Mashariki.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK