TCRA, BASATA Waache Kukandamiza Uhuru wa Maoni

OFISI YA WASEMAJI WA KISEKTA.

TCRA NA BASATA WAACHE KUKANDAMIZA UHURU WA MAONI

JUZI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),ilivitaka vyombo vya Habari vya kielektronic hususan redio Tv na mitandao ya kijamii kutoutumia wimbo wa msanii wa Kizazi Kipya Emanuel Elibariki(Ney wa Mitego) walioutaja kwa jina la Tozo, wakieleza kuwa wamepokea taarifa kutoka baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) kuwa wimbo huo maudhui yake haufai katika jamii.

Sisi ACT Wazalendo,tumeufuatilia na kuusikiliza kwa makini wimbo huo na kujiridhisha kuwa hauna kasoro yoyote ya kimaudhui, Zaidi ya hofu ya watendaji wa serikali juu ya serikali kukosolewa.

Tumejiridhisha pia kuwa hatua hii ya kufungia wimbo wa msanii kwa madai kuwa hauitendei haki jamii kimaudhui ni mwendelezo wa ukandamizaji wa uhuru wa maoni kwa wasanii unaofanywa na basata na kubarikiwa na TCRA

Msanii Ney wa Mitego amekuwa mhanga mkubwa miongoni mwa wengi kwa uhuru wake wa kutoa maoni na kujieleza kupitia nyimbo kuingiliwa kwa kufungiwa nyimbo zake mara kwa mara

Tunalaani hatua hii ya uporaji wa uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 (1).

Sekta ya Mawasiliano, teknolojia ya Habari na Uchukuzi ya ACT Wazalendo, tunalaani vikali kitedndo hicho cha basata kuufungia wimbo huo wa Ney wa Mitego pamoja na TCRA kuiviagiza vyombo vya habari kutoupga wimbo huo.

Tunatambua kuwa Ilani ya ACTWazalendo ukurusa wa 3 imesisitiza kulinda uhuru wa raia kutoa maoni na kutoingiliwa,Tumesisitiza kufuta sheria na kanuni zote kandamizi zilizotungwa na zinazotumiwa na watawala kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na raia kutoa maoni.

Kutokana na msimamo huo tulioubainisha kwenye ilani yetu, ACT Wazalendo kupitia sekta ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi, tunaitaka BASATA NA TCRA .
(i) Kuheshimu uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kwa wasanii kupitia nyimbo hata kama maoni hayo wanayoyatoa kupitia nyimbo hayawapendezi watawala,pasipo kuvunja sheria na katiba ya nchi

(ii)Tunaitaka TCRA na BASATA kutotumia kanuni na sheria vibaya kukandamiza na kuingilia uhuru wa maoni wanaoutumia wasanii kupitia nyimbo,

(iii.) Tunaitaka BASATA kuufungulia mara moja wimbo wa msanii Ney wa Mitego walioutaja kwa jina la TOZO na TCRA kuondoa katazo la wimbo huo kutotumika katika vyombo vya Habari

Imetolewa na:
Mwl Philbert Macheyeki
Msemaji Sekta ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi
ACT Wazalendo
25 Sept, 2022.

Showing 1 reaction

Please check your e-mail for a link to activate your account.

Ukurusa huu unatumia kuki. Kusoma zaidi, angalia Vigezo na Masharti yetuOK